Jeshi
la Polisi nchini linapenda kuutaarifu umma kwamba aliyekuwa Mkurugenzi
wa Upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) Robert Manumba amefikia umri wa
kustaafu kisheria ambao ni miaka sitini (60) katika utendani wake wa
kazi.
Aidha,
katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi amefanya kazi katika
nyadhifa mbalimbali zikiwemo Chumba cha kupokea mashtaka kuanzia mwaka
(1976 – 1977), mwendesha mashtaka wilaya ya Kibondo na Kasulu mkoani
Kigoma, 1977 – 1984), Mkufunzi katika chuo cha polisi Dar es salaam,
(1984 – 1987), Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Magomeni na Kinondoni na
Naibu Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es salaam (1987 – 1993),
Pia,
amewahi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Arusha, ( 1993 –
1995), Mkufunzi mkuu wa Chuo Cha Polisi Moshi ( 1995 – 1996), Mkuu wa
kitengo cha Fraud makao makuu ya upelelezi, (1996 – 1997), Mkuu wa
kitengo cha usalama wa nchi, intelijensia na madawa ya kulevya makao
makuu ya upelelezi (1997 – 2001) na kuwa msaidizi wa mkurugenzi wa
upelelezi wa makosa ya jinai nchini (2001 – 2006). Kuanzia mwaka 2006
hadi anastaafu, alikua Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai
nchini.
Aidha,
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, amemshukuru na
kumpongeza (DCI) Manumba anayestaafu kwa kulitumikia taifa katika
nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi kwa weledi na uwaminifu
mkubwa wakati wote alipokuwa mtumishi ndani ya Jeshi la Polisi.
Pia,
amemtaka kuendelea kuwa msaada kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa
ushirikiano wa namna yoyote ile unaoweza kusaidia kupunguza uhalifu hapa
nchini kwasababu suala la usalama ni taaluma kama zilivyo taaluma
zingine, na taaluma hiyo wanayo watu wachache.
Hata
hivyo, wakati tataratibu wa uteuzi wa mkurugenzi wa upulelezi
ukiendelea, mkuu wa ufuatiliaji na tathimini CID makao
makuu, kamishina Isaya Mungulu, atakua akikaimu nafasi hiyo.