Like Us On Facebook

Mainda aipasua Bongo Movie....Ni baada ya kuwachanganya kimapenzi vigogo wawili wa kundi hilo.

Imebainika kuwa chanzo kikubwa cha kundi lililokuwa na nguvu katika tasnia ya filamu hapa nchini la bongo unity kugawanyika ni Mwanaidi Suka 'Mainda'. 

Chanzo cha habari kilichoomba kuhifadhiwa jina kimeeleza kuwa Mainda amekuwa chanzo kwa sababu wasanii wawili wa kundi hilo wenye nguvu kubwa walikuwa wakigombania  penzi lake.

Kimeendelea kusema kuwa, awali, Ray alikuwa akitoka na msanii huyo lakini ghafla upepo ulibadilika ambapo kiongozi wa ufundi wa kundi hilo alianza kulisarandia penzi la Mainda. 

Inadaiwa kuwa kiongozi huyo wa ufundi ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa wa kuwafuata wafadhili wa kundi hilo alishindwa kumpata mainda ndipo akaamua kuacha kupeleka udhamini ndani ya kundi hilo na hivyo kusababisha kundi kupoteza mwelekeo.
 
''Jamaa alikuwa na nguvu kubwa sana  kuwashawishi viongozi na wafanyabiashara wakubwa kudhamini shughuli za kundi hilo lakini toka mtafaruku huo ulipotokea jamaa amejiweka pembeni'' alisema. 

Aliendelea kusema kuwa,kujitoa kwa kiongozi huyo ndio sababu ya shughuli zilizokuwa zikifanyika na kundi hilo kushindwa kufanyika hivyo kupoteza mwelekeo kwenye jamii.
 
Hata sababu ya kutohudhuria msiba wa baba yake Wema Sepetu ni hiyo kwani wasanii wengi kwa sasa hawana umoja waliokuwa nao mwanzo chini ya Jacob Steven 'JB' ambaye alikuwa hana maringo na alikua mstari wa mbele kuliongoza kundi.
 
Isingekuwa Mainda kuwachanganya Ray na huyo jamaa ambaye alikuwa kinara wa kuwatafuta wadhamini wa kundi hilo lingekuwa na nguvu sana kwa sasa ambapo lipo chini ya TAFF,'' kilisema chanzo hicho.
 
Jitihada za kumpata Ray na Mainda kuzungumzia mpasuko huo zilishindikana kwa kilichoelezwa kuwa wasanii hao wako lokesheni wakiandaa filamu zao.

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari