Like Us On Facebook

HUYU NDIYE MWENYE MKONO AMBAO ULIZIKWA KARIBU NA KIWANDA CHA WACHINA

UKAMILIFU wa binadamu ni pale anapozikwa, kabla ya hapo si kamili! Jumanne Rashid (24), Jumatatu iliyopita aliamka nyumbani kwake, Manzese Dar akiwa mzima wa afya na kuelekea kazini Kiwanda cha Urafiki Plastic Co. Ltd kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Lakini ghafla, ukamilifu wake uliyeyuka baada ya mashine moja ya kiwanda hicho kumkata mkono wote wa kushoto na kuanguka.
Aidha, aliulalamikia uongozi huo kwamba  waliuchukua mkono wake bila kuwashirikisha ndugu zake, wakauzika kienyeji jirani na kiwanda chao, tena bila kumfahamisha yeye mwenye mkono.
Jumatano iliyopita, raia waliuona mkono huo na kulazimika kuwaita Polisi wa Kituo cha Urafiki-Ubungo, Dar  ambao  walipofika, majirani waliwatuhumu Wachina hao ambao ni mabosi wa Jumanne, kuhusika na tukio hilo kwani walikuwa na taarifa za kijana huyo kukatika mkono.

































Baada ya kuufukua mkono huo, polisi walikwenda kumkamata mwekezaji anayemiliki kiwanda hicho cha kutengeneza mifuko ya plastiki aitwaye Lee Slimy na kumhusisha na tukio hilo.
Jumatano iliyopita,  lilipompata Jumanne katika wadi na. 12 katika Jengo la Kibasila, Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam aliongeza zaidi:
“Siku ya tukio niliingia kazini kama kawaida na kuendelea na majukumu yangu, baadaye nikabaini tatizo katika moja ya mashine za kiwanda ambayo ilikuwa imezimwa kutokana na kukatika kwa umeme.
Nikaingiza mkono wa kushoto ndani ya mashine hiyo ili kurekebisha tatizo, lakini ghafla nikashtuka kuona umeme umewaka na mfanyakazi mwenzangu mmoja (hakumtaja) akawasha ile mashine na kilisababisha mkono wangu kukatika hapo hapo.”
Jumanne alisema baada ya tukio hilo alikimbizwa Hospitali ya Palestina, Sinza, Dar kabla ya kuhamishiwa Muhimbili.
 “Iliniuma sana, niliuacha mkono wangu ndani ya mashine nikawa sijui ulipo. Hakuna bosi aliyekuja kuchangia gharama za matibabu. Nashangaa kusikia leo (Jumatano iliyopita) mkono wangu umeonekana ukiwa umezikwa,” alisema kwa masikitiko Jumanne mkazi wa Manzese, Dar.
juzi tulimtafuta kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Komba ili azungumzie suala hilo lakini bila mafanikio.

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari