Like Us On Facebook

HUYU NDIO MSHINDI WA EBSS 2013, AKABIDHIWA KITITA CHA MILIONI 50 ..! CHEKI HAPA


Zawadi kwa mshindi wa mwaka huu ni Milion hamsini[50]ambayo kakabidhiwa jukwaani.


Kinyanganyiro cha kumtafuta Super Star wa Bongo kupitia Epiq Bongo Star Search 2013 kimekamilika alfajiri hii kwenye ukumbi wa Escape 1.

Mashindano haya ambayo kidogo yalichelewa kuanza yalipambwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Barnaba,Makomando,Young Killer,water chilambo,Shaa,Kimbunga na Snura.

Katika mashindano haya ambayo yalikua na jumla ya washiriki watano ambao ni Amina Chibaba,Elizabeth Mwakijambile,Emmanuel Msuya,Maina Thadei na Melisa John,ambao walipita kwa round tatu kisha majaji kuwapunguza watatu na kisha kubakia Emanuel Msuya na Elizabeth Mwakijambile katika Round ya 4 na ya mwisho.


 
Katika round ya mwisho,Emmanuel Msuya ameibuka kidedea na kuwa Mshindi wa Epiq Bongo Star Search 2013,akiwa ni mshiriki anaetokea Jijini Mwanza na kumpokea taji water chilambo ambae alikua mshindi wa mwaka jana.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari