WENYE MSIMAMO
Wanawake
 daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, 
uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, walio makini kwenye matendo 
yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio. 
WAPENDA USAWA
 Aina
 ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake 
wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia 
kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa 
asilimia 50 kwa 50. 
WANAOJUA MAPENZI 
Wanawake
 wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa 
kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa 
wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. 
Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila 
kujali sifa zao za nje au za ndani.
MARAFIKI 
Wanawake
 wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao 
hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na 
kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha 
kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda amani. 
WAPENDA UWAZI 
Aina
 nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na wapenda 
uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio 
cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa 
muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa
 mambo. 
WANAOJITEGEMEA
Wanawake
 wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina ‘naomba 
vocha’ kila siku. Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume wa leo hawapendi 
wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande 
mmoja. WASIO NA PRESHA Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha 
wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo 
yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama 
wapenzi. 
MARIDADI
 Kundi
 lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na 
kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje lakini 
pia ni waelewa wa mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa mwonekano. 
WANAORIDHIKA Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio 
kikubwa kwa wanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu 
wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa 
yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote 
bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.  
WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana."



 
 
 
 
 
 
