Kulwa Kikumba ‘Dude’. |
MSANII wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa mastaa wa kike wengi wanajihusisha na usagaji kutokana na tabia zao za kuiga kila kitu kutoka nje ya nchi.
Akistorisha na paparazi wetu pasipo kuwataja majina, Dude alisema tabia ya usagaji imekithiri kwa mastaa wa kike kutokana na kupenda kuiga kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambayo picha nyingi zinatoka nje ya nchi jambo ambalo linaharibu sifa nzima ya wasanii.
“Tuepuke kuiga vitu ambavyo siyo utamaduni wetu, mastaa tumekuwa tukiiga kila tunachokiona kwenye mitandao kama hiyo tabia ya usagaji Tanzania siyo maadili yetu hayo,” alisema Dude.
--Gpl