Like Us On Facebook

Diamond kuingiza sokoni Jeans,Viatu, Boxer na T. Shirt zenye lebo ya ‘WCB’

Diamond Platinumz anatarajia kuingiza sokoni bidhaa za kampuni yake ya Wasafi Classic, WCB hivi karibuni ambazo ni pamoja na viatu,T.shirt,jeans na mavazi mengine ya wanaume yenye lebo ya WCB. 1170102_653572961330322_1781091457_n Akizungumza jana na Clouds E ya Clouds TV ,Diamond alisema hivi karibuni atatumiwana sample za bidhaa hizo ili azihakiki na hatimaye ziingine madukani. Nikweli tulikuwana na designer tofauti tofauti kutoka wasafi WCB’ lakini kwasasa zitakuwa za kiume tu ,kwa wanawake zitakuwa wachache ambao wanaweza kuvaa nguo za kiume kidogo,kwa wanawake bado nisiwe muongo,lakini zipo tayari. Kwasababu nikiwa China nilikuwa nashughulikia hivyo vitu. Lakini nikifanya chini chini kidogo kwasababu sikupenda vikichelewa halafu mwisho wa siku tuje tupigizane kelele, ‘mbona mulisema hazichelewi mbona zimechewa’, alisema Diamond. Lakini vilitakiwa viwe tayari toka Jumatatu iliyopita,kwasababu nahakikisha quality nzuri isionekane tunafanya tu, ikabidi ichelewe. Kutakuwa viatu,jeans,kutakuwa kuna hadi boxer, T. Shirt, kofia mengi yatakuwa na mchanganyiko mchanganyiko kidogo kwasabubu vitakuwa vya vijana zaidi yaani dizaini kama wasafi tunavyovaa.

---Bongo5
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari