
Mrembo wa haja ambaye jina halikupatikana mara moja, amenaswa akiwa matiti nje baada ya kulewa mchana kweupe na kulizwa mkoba wake kisha kuzua varangati zito,
Varangati hilo lililonaswa na kachero wetu lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya
Sinza- Afrika Sana jijini Dar.

Katika sinema hiyo ya bure, mrembo huyo alishuhudiwa akipigana na
kila mtu aliyekutana naye mbele yake huku akivua nguo kuashiria kuwa
‘pombe si chai’.
Kuna wakati mwanadada huyo alikatiza barabarani bila kujali magari na
nusura agongwe jambo lililosababisha mtafaruku wa foleni huku mwenyewe
akidondoka kama ‘embe dodo’ lililoiva.

Baada ya timbwili hilo kuchukua takriban dakika 35, ilibidi wasamaria wema kuingilia kati na kumshika huku akiwapiga baada ya kuona huenda angeumizwa.

Baadaye watu hao walifanikiwa kumtoa eneo la barabara huku
wakimsitiri kwa kupandisha nguo kufunika nido kisha kumpeleka pembeni na
kumtuliza.
“Kweli pombe siyo chai. Yaani msichana mzuri lakini ona alivyojidhalilisha,” alisema mmoja wa mashuhuda hao.

Source: Global publisher