Mwanamziki mkongwe nchini Nguza Viking aka Babu Seya na mwanaye Papii Kocha, wataendelea na kifungo cha maisha jela baada ya mahakama ya rufani nchini kuitupilia mbali rufaa yao iliyosikilizwa leo
Babu Seya na Papii Kocha
walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na
hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini
Dar ambapo wamekuwa wakikata rufaa mara kwa mara lakini wakagonga
mwamba. Hukumu hii ya rufaa ndiyo ya mwisho kusikilizwa.