Wema akiwa na majonzi wakati wa msiba wa baba yake nyumbani kwao Sinza Mori jijini Dar.
WEMA KUZIMIAChanzo chetu kilisema: “Wema bado mdogo, katika maisha yake hakuwahi kupatwa na msiba mkubwa kama huu, kumpoteza baba yake kipenzi, ni jambo zito ndiyo maana mpaka sasa tunaongea ameshazimia mara tatu, yaani anazimia na kurejewa na fahamu.”
Jumapili saa 7 mchana baada ya kurejewa na fahamu, alisema: “Nimeumia sana kwani huu ni msiba mkubwa kwangu, Baba yangu alikuwa nguzo imara katika maisha yangu, sikuwahi kufikiria kama ningepata msiba mkubwa kama huu.
“Taarifa hizi wakati nazipokea nilijua kama utani lakini yote ni mipango ya Mungu, inaniuma sana,” alisema Wema.
WASIFU MFUPI WA MAREHEMU MZEE SEPETU
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo visiwani Zanzibar, vilevile akawa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, miaka ya 1970 wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwaka 1982, alteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi, wadhifa ambao aliendelea kuushikilia mpaka kipindi cha Awamu ya Pili chini ya Rais Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Kati ya mwaka 2001 na 2006, Balozi Sepetu alichaguliwa kuwa mbunge katika Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM, Zanzibar.
Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi visiwani humo (Zipa).
Machi 27, mwaka huu, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alimteua Balozi Sepetu kuendelea na wadhifa huo wa Zipa kabla ya mauti kumchukua.