Mara
ya kwanza alipotoka katika shindano la BBA 2013, Beverly Osu,
aliwashangaza watu baada ya kukataa kuwa hajafanya mapenzi na mshiriki
kutoka SA, Angelo, licha ya kuwa karibu kila mtu aliona video ambayo
ilisambaa kila kona.
Kwahivi sasa anatengeneza wimbo wake, na alipoulizwa kuhusu video hiyo hiki ndicho alichokisema:
"sijiskii
vibaya kwasababu i was being my self. kwahiyo siwezi kuomba msamaha kwa
mtu yoyote anaehisi nilimuangusha. Wanaishi maisha yao nami naishi
maisha yangu. Tofauti ni kuwa nilikuwa ndani ya lile jumba kuhakikisha
mambo yangu yanenda sawa, mambo ambayo kila mmoja alikuwa akiyafurahia
nikiyafanya. Kama mlikaa kwenye TV zeni kwa siku 91 ili tu kuona makosa
yangu inabidi mjiangalie wenyewe kwasababu watu wana makosa yao na ni
watu wenye makosa tu ndio wenye kugundua haraka makosa ya mtu mwingine.
Sikosoi watu na sidhani kama watu wanatakiwa kunikosoa mimi, vyovyote
utakavyoichukulia mimi bado ni kijana"
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.