Watanzania
wametakiwa kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kuchukia
uhalifu na kuhakikisha taifa linaendelea kuwa la amani, usalama na
utulivu kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Advera Senso alisema hayo wakati akizungumza na mpekuzi wetu kuhusu maadhimisho ya leo ya Siku ya Nyerere.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Advera Senso alisema hayo wakati akizungumza na mpekuzi wetu kuhusu maadhimisho ya leo ya Siku ya Nyerere.
Senso alisema Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi mwenye
msimamo imara, alichukia vitendo vyote vya ubadhirifu, unyanyasaji,
uchochezi wa kidini, kisiasa ikiwa ni pamoja na vitendo vya uhalifu.
Wakati
huo huo maadhimisho ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere yanafanyika kitaifa leo mjini Dodoma yakiongozwa na mwanasiasa
mkongwe, Balozi Job Lusinde.
Mkurugenzi Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Charles Magaya alisema itaongozwa na mmoja wa washirika wa Baba wa Taifa, Balozi Job Lusinde.
"Maadhimisho hayo yataongozwa na mmoja wa washiriki wa
Baba wa Taifa katika kupigania Uhuru wa Tanganyika Mheshimiwa Balozi
Lusinde ambaye pia ni muasisi wa Chama cha TANU," alisema Magaya.
Sambamba
na maadhimisho hayo, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma
imeandaa sinema mbalimbali za Mwalimu Nyerere zitakazooneshwa katika
viwanja vya Nyerere Square.
Magaya aliwataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma kushiriki katika maadhimisho hayo ya kumuenzi Baba wa Taifa.
Hii ni hotuba ya mwalimu Nyerere mwaka 1995