Like Us On Facebook

"TUNAMSHAURI NGASSA AANDAE KABISA GARI LA ZIMA MOTO,TUSIJEMTIA HASARA BURE" SIMBA

                KLABU ya Simba imemtaka kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, aandae kabisa gari la kuzima moto kwenye nyumba zake kwa kuwa ina uhakika mchezaji huyo hataweza kutimiza ahadi yake ya kufunga au kutoa pasi ya bao.
Simba na Yanga zinakutana keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar na Ngassa ameahidi asipofunga au kutoa pasi itakayozaa bao, basi atazichoma moto nyumba zake tano.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema hawana hofu na Ngassa na kwamba hana hata historia ya kuifunga Simba, hivyo cha msingi aandae zima moto haraka ili kuepuka hasara mapema.

“Siwezi kusema hatatufunga kwa kuwa ni majaaliwa ya kila mtu jinsi Mungu alivyompangia lakini sisi hatuna hofu naye, atambue kuwa hajawahi au hana historia ya kuifunga Simba, ila tunamshauri aandae zima moto mapema, tusijemtia hasara bure,” alisema Kamwaga.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari