
Hit maker wa Roho yangu, Rich Mavoko amesema ameanza kupata mafanikio makubwa katika muziki wake baada ya kununua gari aina ya Nissan pamoja nyumba ambayo bado anaendelea kuijenga mkoani Morogoro.

Nyumba ya Rich Mavoko ambayo ipo Morogoro “Sina cha kusema muziki unalipa, nyumba yangu ni kubwa sana na pia nimejaribu kuonyesha ni mafanikio gani ambayo nimeyapata mpaka sasa. Kwahiyo namshukuru Mungu na mashabiki ambao wananiwezesha,” amesema Mavoko.
