Babu,mmiliki wa gesti |
Tukio hilo lilitokea Oktoba 26, mwaka huu maeneo ya Toangoma jijini Dar, baada ya waandishi wetu kuzinyaka taarifa hizo na kuzifikisha kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Chande Mohammed aliyefika eneo hilo na polisi.
Awali, ili kujiridhisha, mmoja wa mapaparazi wetu alijifanya mteja na kufika katika gesti bubu hiyo, kisha kupangisha chumba kwa malazi ya siku moja kwa malipo ya shilingi 3000 tu lakini pasipo kuandikisha mahali popote.
Baadhi ya watu waliokamatwa kwenye msako wa machangudoa |
“Ningefuata utaratibu, manispaa isingeniruhusu kutokana na ubora wa vyumba vyenyewe, kama mnavyoona. Pia njaa tu jamani ndiyo imenifanya nianzishe gesti hii,” alisema mzee Abdullahim.
Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa huo, alisema kuwa mzee huyo ana kesi ya kujibu kwa kukiuka taratibu za kibiashara zilizowekwa na halmashauri na kumuamuru aifunge gesti hiyo mara moja huku akiahidi kumpeleka Baraza la Kata kwa ajili ya masikilizano ya awali.
Timu yetu iliwaachia msala wao na kuendelea na oparesheni nyingine ambapo walifanikiwa kuwanasa machangudoa wakijiuza jirani na mtaa huo huku ikielezwa kuwa, wateja wa madadapoa hao hupelekwa katika gesti bubu ya mzee huyo kwa vile ni bei poa.