Like Us On Facebook

MAMA DIAMOND AINGILIA PENZI LA DIAMOND, WEMA

Habari za chini ya kapeti zilitonya kuwa baada ya kuambiwa na kuoneshwa picha za Diamond akiwa kimahaba na Wema alikuja juu akidai kuwa hamtaki Wema kwa kuwa anamkubali zaidi Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Akizungumza  nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar wikiendi iliyopita, bi’mkubwa huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na kuona picha katika mitandao ya kijamii.
“Kuhusu Nasibu (Diamond) kurudiana na Wema, nasikia tu na kuoneshwa picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa tamko,” alisema mzazi huyo.
Mapaparazi wa Ijumaa Wikienda kadiri walivyozidi kumchimba mama mkwe huyo wa Wema ni jinsi gani anavyojisikia kuhusu tabia ya kubadilisha wanawake kama nguo, ikizingatiwa yeye ni mzazi haoni kama mwanaye anamfedhehesha alisema kuwa hayo ni maisha yake.
“Hayo ni maisha yake na mwenyewe kwa kuwa ameshazoea kuonekana katika magazeti kila wakati mi niongee nini wakati ndiyo maisha aliyojiwekea,” alimalizia kusema.

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari