Askari wakiupakia mwili wa marehemu huku wananchi walio na huzuni wakishuhudia
(Picha Na George Almas)
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa maiti hiyo imeonekana baada ya kuhisi harufu mbaya ikitokeo jirani kabisa na makazi yao.Baada ya kuhisi harufu hiyo walianza kutaka kujua harufu inatoka wapi na inatokana na nini ndipo walipo fika eneo hilo na kukuta mwili huo ukiwa ndani ya mfuko.
Wananchi hao wanasema maiti hiyo imeharibiaka sana, lakini mpaka sasa haijajulikana kuwa maiti huyo ni nani.Baada ya kuona mwili huo wananchi walitoa taarifa polisi ambao walifika na kuuchukua mwili wa marehemu.