Like Us On Facebook

KAJALA ANASWA AKIWA AMEVAA KANGA MOKO KITAA

KATIKA hali ya kushangaza, staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja  amenaswa akiwa ametinga khanga moja na kuwaacha watu midomo wazi.
Kajala alinaswa na kamera yetu maeneo ya Kigogo jijini Dar ambapo watu kibao walionekana kumzunguka na kuhoji kulikoni staa huyo ambaye amezoeleka kutika pamba kali, aonekane na vazi la khanga?




Akizungumza na PAPARAZI, Kajala alisema alilazimika kutinga khanga hiyo kuendana na matakwa ya filamu yaliyomtaka kuvaa vazi hilo na kuonesha mazingira ya uswahilini hivyo watu waliomzunguka walikuwa hawajui nini kinaendelea.



“Nilipoambia naigiza sinema ya Kigodoro nilishtuka sana lakini mwisho wa siku nilikubali kwa kuwa mimi ni msanii naweza kubadilika kivyovyote na nina imani mashabiki wangu wataniona kivingine, humo ni full mcharuko,” alisema Kajala.

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari