Wanaume hao waliokuwa wamejihami , waliwasimamisha madereva na
kuwaamrisha kuondoka kutoka katika magari yao kabla ya kuwapiga risasi
na kuwaua.
Jimbo hilo la Kaskazini mwa Nigeria liko chini ya sharia ya hali ya hatari, huku Boko Haram wakiwa vitani na serikali kutaka utawala wa kiisilamu.Walioshuhudia tukio hilo waliambia BBC kuwa wanaume hao walikuwa wanachama wa Boko Haram, ingawa kundi hilo bado halijatamka chochote kuhusu mauaji hayo.
Kundi hilo huwalenga raia na wanajeshi kwa mashambulizi ikiwemo shule na makabiliano ya mara kwa mara na jeshi la taifa.
Shambulizi la hivi karibuni, lilifanyika Jumapili, asubuhi karibu na mji
wa Logumani, ambao hauko mbali sana na mpaka na Cameroon.
Walionusurika shambulizi hilo walisema kuwa washambuliaji walivaa nguo
za jeshi na walikuwa wanaendesha pikipiki kabla ya kuwashambulia
waathiriwa.
"Takriban wanaume 9 walituamuru kuondoka kwenye magari yeu na kulala chini,’’ alisema mwanamume
"Waliwaua watu 5 kwa kuwapiga risasi na kasha kuwanyonga wengine 14
kabla ya mtu mmoja kuwapigia simu na kuwambia kuwa wanjeshi wanakuja.’’
Alisema washambuliaji baadaye walitoroka na kujificha msituni kwa pikipiki zao.
Manusura mwingine alisema kuwa alisikia mtu aliyekuwa karibu naye
akiuawa kwa kisu. Alisema ana uhakika kuwa washambuliaji walikuwa Boko
Haram kwa sababu ya kuwa na ndevu.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo alisema kuwa ni jambo la kawida kwa polisi
kuweka vizuizi barabarani hasa katika maeneo yenye misukosuko na huenda
washambuliaji waliiga mbinu hioyo ya jeshi ili kuwanasa waathiriwa. I,
Boko Haram limezua mgogoro mkubwa wa kisiasa Nigeria tangu mwaka 2009,
nia yao kuu ikiwa kuunda utawala wa kiisilamu, hasa katika maeneo ya
kaskazini mwa nchi
Kundi hilo limelaumiwa kwa mashambulizi kadhaa ambao yamesababisha takribna vifo 2,000 tangu mwka 2011.