Like Us On Facebook

HUYU NDIYE BIBI ALIYEZINDUKA BAADA YA KUKAA SIKU 6 NDANI YA JENEZA

Bibi Li Xiufeng baada ya kuzinduka toka kuzimu

Bibi mmoja wa nchini China amewashtua ndugu na majirani zake baada ya kutangazwa kuwa amefariki dunia na kupelekea maandalizi ya mazishi yake kufanyika lakini alizinduka na kurudi duniani siku ya sita akitoka ndani ya jeneza.


Bibi Li Xiufeng mwenye umri wa miaka 95 aligunduliwa na majirani zake akiwa kitandani chumbani kwake akiwa hapumui na haonyeshi dalili yeyote ya kuwa hai.

Tukio hilo lilitokea wiki mbili baada ya bibi Li kuteleza na kuanguka njiani na kupelekea kupata majeraha kichwani kwake.

Baada ya majirani kumkuta chumbani kwake akiwa hapumui, walijaribu kumzindua lakini ilishindikana. Bi Li alikuwa hapumui na wala haonyeshi dalili yeyote ya uhai lakini mwili wake haukuwa wa baridi. Kwa fikira zao na majaribio machache waliyoyafanya, majirani walitangaza kuwa bibi Li amefariki dunia.

Mwili wa bi Li ambaye alikuwa akiishi peke yake akipewa kampani na majirani, uliwekwa kwenye jeneza ndani ya nyumba yake na kwa kufuata taratibu za tamaduni za China, jeneza halikufunikwa liliwachwa wazi juu ili kuwapa nafasi watu kuuaga mwili wa bi Li.

Siku ya sita, majirani walipoenda kuuangalia mwili wa bi Li kabla ya kuuzika rasmi siku iliyofuatia, walishangazwa kukuta mwili haupo ndani ya jeneza.

Msako mkali kijijini ulianza kuutafuta mwili wake na mazingira yanayoizunguka nyumba yake. Baada ya muda watu walishangazwa kumkuta bi Li akiwa jikoni anapika.

"Nililala kwa muda mrefu sana, baada ya kuamka nilihisi njaa kali ikanibidi niingie jikoni kupika kitu cha kula", alisema bi Li alipohojiwa na majirani zake.

Madaktari walisema kuwa kitaalamu bi Li alipatwa na "kifo cha bandia" 'artificial death', ambacho huelezewa kuwa mtu huwa hapumui lakini mwili wake huendelea kuwa wa moto.

"Utamaduni wa kuhifadhi mwili ndani ya nyumba kwa siku kadhaa ndio uliookoa maisha ya bi Li, kama si utamaduni huo bi Li angekuwa ameishazikwa kweli zamani", alisema mmoja wa Madaktari waliomfanyia uchunguzi bi Li baada ya tukio hilo.

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari