Kwa mujibu wa shuhuda wetu, vigogo hao walihudhuria harusi hiyo ya Malumbo Mangula aliyefunga ndoa na msichana ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
Vigogo waliokuwepo ukumbini humo ni pamoja na marais wawili wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi ‘Mzee Ruksa’ na Benjamin Mkapa.
Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wassira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
“Ni vigumu kuwaona viongozi kama hawa wakiwa pamoja kwenye sherehe isiyokihusu chama wala serikali au msiba wa kitaifa, ndiyo maana kila mtu anawazungumzia wao,” alisema shuhuda huyo.
Mbali na kuzua gumzo, wengine walishangazwa na ulinzi uliokuwepo katika harusi hiyo na kuufananisha na ule wa ikulu.