MWENDESHA bodaboda ambaye alifumaniwa na mke wa mtu hivi karibuni
huko Kigamboni-Kibada, Dar, maarufu kwa jina la Chidi anasakwa kwa udi
na uvumba baada ya kuripotiwa kumshushia kipigo mzazi mwenziye
aliyejitambulisha kwa jina moja la Husna.
Mke wa mtu (kushoto) akiwa na dereva bodaboda aitwaye Chidi baada ya kufumaniwa.
Tukio la kipigo lilitokea Septemba 26, mwaka huu maeneo hayo ya
Kibada ambapo chanzo kilibainisha kuwa Chidi alipata wivu wa mapenzi
baada ya kusikia tetesi kuwa mzazi mwenzake ametangaza kuwa hana mpenzi
kufuatia jamaa huyo kufumaniwa.Katika kuchimba zaidi tukio hilo, ilidaiwa kuwa Chidi alimtelekeza mwanamke huyo na mtoto wake mdogo aitwaye Adam na kwenda kuishi na mke wa mtu ambaye ndiye aliyeshikwa naye ugoni.
Akizungumza Husna alidai kuwa amekuwa akipeleka malalamiko kwa Chidi na ndugu zake kuhusu huduma hafifu kwa mtoto wake lakini mara zote jamaa huyo alikuwa mkali na kufikia hatua ya kutoa fedha kidogo.
“Baadaye nilikuja kugundua kwa nini hatoi fedha ya matumizi baada ya kusoma kwenye gazeti kuwa Chidi amenaswa ugoni na mke wa mtu.
Alisema tangu Chidi ashikwe ugoni na mke wa mtu, amebadilisha jina na kujiita Supastaa huku akitembea na nakala ya gazeti ambalo lilichapisha habari ya yeye kufumaniwa.
Alisema Husna alipoamua kukaa pembeni ndipo Chidi akamfuata na kumpa kichapo hivyo anasakwa na polisi Kigamboni kwa jalada la kesi namba KBA/RB/549/2013-TAARIFA.