Like Us On Facebook

BREAKING Newzzzz: MTANGAZAJI WA ITV JULIUS NYAISANGAH 'UNCLE J' AFARIKI DUNIA.

                                              julius nyaisanga wa katikati pichani
  HABARI zilizotufikia kutoka mkoani Morogoro ni kwamba Mtangazaji Mkongwe nchini, Julius Nyaisangah 'Uncle J' ameaga dunia. Mpaka mauti yanamfika, Marehemu Nyaisangah alikuwa Mhariri Mtendaji wa Abood Media iliyopo mkoani Morogoro. Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika kituo cha Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na katika Kituo cha Redio One ambapo alikuwa Mkurugenzi. Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika japo marehemu alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!  Taarifa zaidi zitawajia baadaye.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari