Like Us On Facebook

BARCA WATAKA KUMNG'OA JANUZAJ MAN UNITED, MWENYEWE AITOLEA NJE UBELGIJI

                  KLABU ya Barcelona iko tayari kumchukua Adnan Januzaj kutoka Manchester United iwapo atakataa ofa ya kuongeza Mkataba. 
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Sunderland Jumamosi.
Lakini Barca imekuwa ikifuatilia kipaji cha mwanasoka huyo tangu hajajiunga na United kutoka Anderlecht mwaka 2011. Barca wanaamini sana kwamba Januzaj atahamia tu Nou Camp wakati atakapomalizia miezi minane iliyobaki katika Mkataba wake. 
Premature? Adnan Januzaj has already attracted the top European clubs after just one standout performance
Amekomaa? Adnan Januzaj tayari amezivutia klabu kadhaa Ulaya
Hot property: Januzaj pictured taking a stroll through Manchester on Sunday
Yuko juu: Januzaj akitalii mitaa ya Manchester Jumapili

Pamoja na Mbelgiji huyo kusema ana furaha United, lakini imeelezwa amekuwa akihisi kutokubalika wakati fulani. Mazungumzo ya Mkataba mpya yalikufa baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson Mei mwaka huu kabla ya kufufuka hivi karibuni.
Wakala Dirk de Vriese alionya wiki iliyopita: "Siwezi kusema timu zipi zina nia naye, lakini naweza kukuambia klabu kadhaa Ulaya zinammezea mate,". 
United inatumai kupandishwa kwa Januzaj chini ya David Moyes na ofa ya Mkataba mzuri wa muda mrefu vitakuwa vishawishi tosha vya kumbakiza mchezaji huyo.
Lakini wanahofia Januzaj na De Vriese 'wanaburuzwa' na baba wa mchezaji huyo. Moyes hivi karibuni amejaribu kumuweka karibu mchezaji huyo.
Double: He scored both goals as United game from behind to beat Sunderland at the Stadium of Light
Mbili: Alifunga mabao yote United ikishinda 2-1 dhidi ya Sunderland Uwanja wa Light

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Anderlecht, Jean Kindermans, mtu ambaye anastahili sifa za kuibua kipaji hicho, alionya jana usiku kwamba Januzaj Snr anataka kuwa na kauli ya mwisho juu ya mwanaye kama atabaki United au ataondoka na pioa juu ya timu ipi ya taifa ataichezea.
Akiwa amezaliwa Ubelgiji na wazazi Kosovo na Albania, Januzaj anaweza kuchezea nchi kadhaa na kocha wa Ubelgiji, Marc Wilmots amechukua hatua ya kwanza kwa kumuita mchezaji huyo kikosini mwake kwa ajili ya mechi zijazo za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Croatia na Wales.
Lakini ombi hilo lilikataliwa, huku Januzaj akiwataka mabosi wa Old Trafford kujibu kwamba anataka muda zaidi wa kufikiria mustakabali wa utaifa wakle.
Youngster: Januzaj has only featured in a handful of games so far this season
Nyota kinda: Januzaj anatarajiwa kupata nafasi zaidi kikosini United msimu huu

Januzaj alisema: "Kwa sasa, soka ya kimataifa si jambo ninalofikiria kwa kiasi kikubwa. Nafahamu kwamba, kwanza natakiwa kuelekeza fikra zangu juu ya kile ninachokifanya United, kwa sababu hiyo ndiyo muhimu zaidi katika soka yangu kwa sasa.’
Adna Januzaj
Adnan Januzaj
Anaburuzwa: Inaonekana baba wa kinda huyu mwenye umri wa miaka 18 ndiye mwenye maamuzi juu ya mustakabali wa Januzaj
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari