PAMOJA na kumkosa mchezaji ghali duniani, Gareth Bale, lakini mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani, Cristiano Ronaldo alitosha kuipa pointi tatu Real Madrid usiku huu, baada ya kufunga mabao yote katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Elche.
Bale atarejea katika mechi ya nyumbani na Atletico Madrid Jumamosi wakati leo Ronaldo, ameendelea kuiweka Real karibu vinara wa La Liga.
Ronaldo alifunga mabnao hayo katika dakika za 51 na dakika ya sita ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90, wakati bao la kufutia machozi la Elche lilifungwa na Richmond Boakye dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimua dakika 90.
Kikosi cha Elche kilikuwa: Elche: Manu Herrera; Damián, Botía, Lombán, Albácar; Rubén Pérez, Carlos Sánchez; Stevanovic, Coro, Fidel na Boakye.
Real Madrid: Diego López, Pepe, Ramos, Coentrão, Khedira, Ronaldo, Benzema, Arbeloa, Modric, Di María na Isco.
Raha: Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Madrid bao la pili
Moja zaidi: Cristiano Ronaldo akishangilia na wachezaji wenzake
Weka kule: Real Madrid ilicheza bila mchezaji ghali duniani, Gareth Bale
Beki wa Elche, Botia (kushoto) akikabiliana na mshambuliaji Mfaransa wa Real Madrid, Karim Benzema