KLABU ya Arsenal itamenyana na wapinzani wao katika Jiji la London, Chelsea katika Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup baada ya kuitoa West Brom kwa penalti 4-3 Uwanja wa Hawthorns.
Mechi hiyo imeisha kwa sare ya 1-1 usiku huu, lakini penalti walizokosa Morgan Amalfitano na Craig Dawson zinawasongesha mbele Gunners.
Mbele: United imesonga mbele kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Liverpool Uwanja wa Old Trafford
RATIBA KAMILI RAUNDI YA NNE CAPITAL ONE
Sunderland v Southampton
Leicester City v Fulham
Birmingham City v Stoke City
Manchester United v Norwich City
Burnley v West Ham United
Arsenal v Chelsea
Tottenham v Hull City
Newcastle v Manchester City
Mechi zote zitachezwa Jumanne ya Oktoba 29 na Jumatano ya Oktoba 30.
Manchester United baada ya kuwatoa wapinzan wao, Liverpool watamenyana na Norwich nyumbani katika Raundi ya Nne.
Bao pekee la Javier Hernandez mapema kipindi cha pili katika ushindi wa 1-0 Old Trafford, linawakutanisha Mashetani Wekundu na The Canaries Oktoba 28.
Birmingham iliyowatoa mabingwa watetezi Swansea kwa mabao 3-1 watacheza tena nyumbani katika 16 Bora, safari hii wakimenyana na timu ya Mark Hughes, Stoke.
Licha ya kupangiwa wapinzani wagumu, lakini The Blues bado wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa tena taji walilolitwaa mwaka 2011, na United ikiwa timu nyingine inayopewa nafasi pia baada ya kupangiwa Norwich.
Katika mechi nyingine, Newcastle itaikaribisha Manchester City Uwanja wa St James Park baada ya kuwatoa Leeds, wakati Hull wataifuata Tottenham siku kadhaa baada ya kucheza mechi ya Ligi Kuu, Uwanja wa White Hart Lane.
Timu isiyo na kocha kwa sasa, Sunderland itamenyana na Southampton, wakati West Ham watakwedna Kaskazini kumenyana na Burnley.
Fulham ya Martin Jol itaifuata Leicester kusaka nafasi ya Robo Fainali.
MIKWAJU YA PENALTI
West Brom: Reid (penalti ya kwanza) amefunga, Rosenberg amefunga, Morrison amefunga, Dawson amekosa, Amalfitano amekosa
Arsenal: Bendtner amefunga, Gnabry amekosa, Olsson amefunga, Akpom amefunga, Monreal amefunga
Arsenal imeifunga West Brom kwa penalti 4-3
Arsenal iliendeleza wimbi la ushindi kwa kuitoa kwa matuta West Brom Uwanja wa The Hawthorns na kuingia Raundi ya Nne.
Eisfeld aliifungia Arsenal dakika ya 61 kabla ya Berahino kusawazisha dakika ya 71.
Kikosi cha West Brom kilikuwa: Daniels, Reid, Popov, Lugano, Dawson, Sinclair, Dorrans, Mulumbu/Morrison dk91, Berahino/Amalfitano dk101, Long/Rosenberg dk91, Sessegnon
Arsenal: Fabianski, Mertesacker, Vermaelen, Monreal, Jenkinson, Arteta/Bellerin dk95, Miyaichi, Gnabry, Hayden/Kris Olsson dk84, Bendtner, Eisfeld/Akpom dk82.
Ya ushindi: Nacho Monreal akiifungia Arsenal penalti ya ushindi
Shangwe: Monreal na wachezaji wenzake wa Arsenalwakishangilia
Kazi nzuri: Arsene Wenger akizungumza na Nicklas Bendtner kabla ya kupiga penalti yake
Thomas Eisfeld akiifungia bao la kwanza Arsenal
Thomas Eisfeld akiondoka kushangilia bao lake
Amerejea: Nicklas Bendtner alikuwa mwiba usiku huu The Hawthorns
Mwonekano mpya: Mdenmark amekuja kwa staili ya nywele za David Beckham
Pongezi: Bendtner na Eisfeld wakipongezwa na wachezaji wenzao