Msanii anaekuja kwa kasi ya ajabu katika industry ya bongo muvie GETRUDE BAZIL MUSHI hivi karibuni alifanya 'KUFURU' baada ya kufanya birthday party ya kufa mtu ndani ya mgahawa wa CHICKEN HUT uliopo Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuudhuliwa na mastar kibao wa tasnia iyo ya filamu nchini. Akizungumza alisema anafuraha sana kutimiza miaka kadhaa apa duniani kwani sio wote waliobahatika kufika kama alipofikia yeye ivyo hana budi zaidi ya kumshukuru Mungu na kusherehekea na marafiki zake... Habari chini ya kapeti zinasema pati iyo ilimgharimu zaidi ya milioni mbili kwani watu walikula, walikunywa hadi kusaza... Happy belated birthday GETUCELEBRITY Mwenyez Mungu akupe miaka mingi zaidi na yenye heri duniani...