Like Us On Facebook

MASOGANGE, MELISA WAAMUA KUWATAJA WALIOWATUMA MZIGO WA UNGA BAADA KIBANO

BAADA ya warembo hao kukamatwa ilielezwa kuwa walikuwa wakigoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.

Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema aliyewatuma.


“Unajua Sauzi (Afrika Kusini) huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya. Jamaa (polisi) wana kila aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.

“Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.

“Kwanza utaanzia kwenye chumba kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.

“Wakishakuingiza mle ndipo utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung’ata mwili mzima, zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.

“Kama bado ukijifanya mbishi au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja ndogo kwenye waya wa umeme.
“Si unajua tena waya wenye umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea.

“Kinachofuata ni mtu kupigwa shoti kali ya umeme ambapo lazima utasema tu.
“Hicho ndicho kilichowapata akina Masogange kama wanavyofanyiwa Wabongo wengine wanaokamatwa Mitaa ya Rissik hapa Johannesburg.




“Baada ya mateso hayo, waliwataja waliowatuma mzigo huo wa unga aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8,” kilisema chanzo hicho ambacho ni Mbongo ambaye kwa sasa ni mkazi wa Mtaa wa Rissik, Johannesburg, wanapoishi Wabongo kwa kuungaunga aliyewahi kukumbwa na mkasa kama huo.



Habari za ndani zilidai kuwa baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao waliwataja watu wawili waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni mtoto wa kigogo ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina lipo).



Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wa mkubwa ni mjanja wa mjini ambaye alihusika kushughulikia kusafirisha mwili wa msanii Albert Mangweha ‘Ngwea’ aliyefia Johannesburg Juni, mwaka huu.



Ilivuja kuwa mwingine aliyetajwa na akina Masogange ni mfanyabiashara maarufu Bongo anayesafiri nje mara kwa mara huku jina la ‘mtoto wa mjini’ Mangunga likitajwa zaidi hata na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe.



Kamanda wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kupewa majina hayo lakini akaliomba gazeti hili kutoyachapisha kwa sasa kuepuka kuvuruga ushahidi.



Baada ya polisi wa upelelezi na wale wa kimataifa (Interpol) kujiridhisha na maelezo ya mabinti hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya pili Agosti 19, mwaka huu chini ya ulinzi mkali kama ule ‘anaowekewaga’ Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anapofikishwa kwenye mahakama mbalimbali nchini kwa kesi zake za madai ya uchochezi.



Habari kutoka Sauzi zilieleza kuwa akina Masogange walipandishwa tena kizimbani hivi karibuni ambapo tayari kesi yao imeanza kuunguruma ikielezwa kuwa endapo watakutwa na hatia watakula mvua ya kifungo si chini ya miaka 10 kwa sheria za nchi hiyo.


Masogange na Mellisa walinaswa nchini humo Julai 5, mwaka huu wakiwa na mabegi sita yaliyokuwa na mzigo huo wa unga.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari