Like Us On Facebook

MASOGANGE AANGUSHIWA PATI LA NGUVU BONGO



     WAKATI msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ akihenyeka nchini Afrika Kusini kwa kesi ya madawa ya kulevya, hapa Bongo baadhi ya mashosti zake wakiongozwa na Jacqueline Wolper hivi karibuni walimfanyia pati.
Pati hiyo ambayo waalikwa wengi siyo mastaa walikunywa, wakala na kucheza muziki, ilikuwa ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Masogange ila kiwanja ilipofanyikia ilifanywa siri.
Mmoja wa watu waliohudhuria sherehe hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alilitonya gazeti hili kuwa pati hiyo haikuwa na mualiko wa watu wengi lakini ilifana huku keki kubwa ikiwa imetolewa na Wolper na kuandikwa; Happy Birthday Masogange, from da best Wolper.
 “Ilikuwa ni pati ya kiaina, watu walishangweka kiaina ila kuna wakati walionyesha nyuso za simanzi pale walipokumbuka kuwa mhusika yuko kwenye matatizo. Ingenoga zaidi  angekuwepo lakini ndiyo hivyo tena, Mungu atamsaidia,” alisema mtoa habari huyo.
Katika kuonesha sherehe ilivyokuwa, Wolper kupitia ukurasa wake wa Instergram alitupia picha ya hafla hiyo na kuwafanya baadhi ya wadau kushangaa kwani hawakutarajia kufanyika kwa pati hiyo bila ya uwepo wa mwenzao.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumpata Wolper kupitia simu yake ya mkononi ili aizungumzie pati hiyo lakini hakuweza kupatikana.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari