Like Us On Facebook

LIVERPOOL YANG'ARA YATOA MENEJA BORA RODGERS,NA MCHEZAJI BORA STURRIDGE! WA MWEZI

           WADHAMINI wa Ligi Kuu England, Barclays, leo wametangaza waliozoa Tuzo ya Mwezi Agosti ya Ligi hiyo ya Meneja na Mchezaji Bora na wote wanatoka Liverpool.
Meneja Bora ni Brendan Rodgers na Mchezaji Bora ni Straika Daniel Sturridge.
Kwa sasa Liverpool ndio Vinara wa Ligi Kuu England baada ya kushinda Mechi zao zote 3 za mwanzo kwa Bao 1-0 katika kila Mechi na Mfungaji wa Bao zote hizo 3 ni Daniel Sturridge.
Liverpool walianza Ligi kwa kuzifunga Stoke City na Aston Villa Mwezi Agosti na Man United Mwezi Septemba.
Hii ni mara ya Pili kwa Brendan Rodgers kutwaa Tuzo hii na ni mara ya kwanza kwa Sturridge.
Meneja ambaye anaongoza kwa kutwaa mara nyingi Tuzo hii ni Sir Alex Ferguson aliekuwa Manchester United alietwaa mara 27 akifuatiwa na Arsene Wenger wa Arsenal mara 12 na David Moyes, ambae sasa yupo Man United, alipokuwa Everton mara 10.
Kwa upande wa Wachezaji, wanaoongoza kwa kutwaa mara nyingi ni Wayne Rooney, Robin van Persie na Steven Gerrard ambao wote wametwaa mara 5 kila mmoja lakini Mchezaji pekee aliewahi kuitwaa Mara nyingi katika Msimu mmoja ni Ashley Young alietwaa Mara 3 kwenye Mwaka 2009 akiwa na Aston Villa.
Manchester United ndio inaongoza kwa kutoa Washindi wengi wa Tuzo hii.
MAMENEJA WALIOTWAA MARA NYINGI:
1 Alex Ferguson Mara 27
2 Arsène Wenger 12
3 David Moyes 10
4 Martin O'Neill 8
Harry Redknapp
6 Rafael Benítez 6
Bobby Robson
8 Kevin Keegan 5
9 Sam Allardyce 4
10.Carlo Ancelotti
11.Roy Hodgson
12.Joe Kinnear
13.Gordon Strachan
14 Alan Curbishley 3
15.Gérard Houllier
16.José Mourinho
17David O'Leary
18.Stuart Pearce
-SOKAINBONGO
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari