Like Us On Facebook

KIBAKA AUMBUKA...!!! BAADA YA KUIBA SIMU WIKI MOJA BAADAE SIMU YAITA TUMBONI.



Kijana mmoja mkazi wa kitongoji cha DDC Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya, Mkoani Mbeya Bwana GOODSON MWASYOGE amejikuta yupo katika wakati mgumu baada ya kuiba simu ya mfanyabiashara wa eneo hilo. Baada ya wiki moja kuiba hiyo simu imekuwa ikilia tumboni na kuchukua kama dakika kumi na tumbo lake kuvimba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Bwana ASIFIWE MWAKALONGE amethibitisha kwa tukio hilo akiwa sambamba na mjumbe Bwana MOHAMMED SAID.




Wakati huo huo Kaka wa muhanga wa tukio hili Bwana DANIEL MWASYOGE akiwa na Mama mzazi Bi CHRISTINA MWAKALONGE amemtaka aliyeibiwa simu kumsamehe kijana wao kwa kosa alilolifanya naye amekiri kutenda tukio hilo na anaomba msamaha kuwa abilisi alimpitia tuu hakuwa na tabia ya wizi na baadhi ra wananchi wa mtaa huo wanashangaa.

Kijana GOODSON ni mmoja wa wafanyakazi wa Machinjioni maarufu kama Butchery Mbalizi.



Hili jambo ni FAIDA kwani ni fundisho kwa vijana ambao hupendelea tabia ya kusogeza mali katika jamii na kusababisha Janga la Umasikini kuendelea kuchukua nafasi.

Na HASARA yake M wenye mali yake atachukuliwa/kutafsiriwa ndivyosivyo ndani ya jamii endelea kufuatilia matandao huu ambapo utakuletea taarifa zaidi kwa njia ya picha.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari