Mwanamuziki Nana Richard Abiona 'Fuse ODG' akiwapagawisha wakazi wa jiji la Dar.
..Akicheza kiduku na mmoja wa mashabiki.
...Akipiga saluti kwa mashabiki waliofurika katika Viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama usiku wa kuamkia leo.
...Fuse ODG wakati akipanda stejini kufanya makamuzi.
MWANAMUZIKI Nana Richard Abiona maarufu kwa jina la Fuse ODG kutoka nchini Uingereza, usiku wa kuamkia leo amewapagawisha wapenzi wa burudani jijini Dar es Salaam kwa shoo kali aliyopiga. Fuse ODG alifanya makamuzi ya nguvu na kuwapa raha mashabiki waliofurika katika Viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii hasa alipoimba nyimbo zake kali mbili za Azonto aliyomshirikisha msanii wa Ghana,Tiffany pamoja na Antenna aliyofanya na Wyclef Jean.