Like Us On Facebook

BINTI ALIYEACHWA NA MZEE MAJUTO AKIMBILIA BAKWATA KUMSHITAKI MZEE MAJUTO...


                SIKU chache baada ya ndoa ya supastaa wa vichekesho Bongo, Amir Athuman ‘Mzee Majuto’ kuvunjika, mke aliyeachika amekimbilia Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) kutoa malalamiko yake.
Rehema Omar (20) ndiye mke aliyeachwa na Mzee Majuto, Septemba 14, 2013 alikimbilia Makao Makuu ya Bakwata Wilaya ya Kinondoni yaliyopo Hananasif, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa msichana huyo, mambo aliyoyazungumza kwenye ofisi hiyo ni matatu, kwanza kutopewa talaka baada ya kuachika.
Akasema akimuuliza Mzee Majuto kuhusu talaka yake anamwambia amempa mwanamke mmoja aitwaye Rehema amfikishie, akahoji:  “Kwani huyo Rehema ndiye aliyenioa?”
Pili, akasema wakati anakaribia kufunga ndoa, mzee huyo alimwachisha kazi mahali na pia alimhamisha kwenye chumba alichopanga.
Tatu, akasema kutokana na hayo yote anaomba alipwe fidia ya fedha kwa sababu ya usumbufu alioupata.
Rehema akasema kutokana na malalamiko yake, viongozi wa Bakwata walimpa barua ya kumfikishia Mzee Majuto yenye kichwa cha habari cha WITO.
Mzee Majuto anatakiwa kufika bila kukosa kwenye ofisi hizo, Septemba 23, mwaka huu ambayo itakuwa Jumatatu ili shauri lake na mwanamke huyo lizungumzwe.
Juzi, tulimpigia simu Mzee Majuto lakini muda wote iliita bila kupokelewa.
 Kwenye utetezi wake, mzee huyo alisema alimwacha mwanamke huyo baada ya kugundua hajatulia
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari