Tuzo kubwa ya siku ya Mchango kwenye Jamii (Social Impact) imechukuliwa na Adam Anthony ambaye ni mkurugenzi wa DAELIT Group anayejihusisha na masuala ya mazingira.
Akiongea na Bongo5 mara baada ya kupata tuzo hizo, Adam amesema pamoja na kuwa na furaha kubwa kushinda tuzo hiyo, bado anahitahi kujitumza zaidi kwakuwa jamii itategemea mambo makubwa kutoka kwake. “Wakati mwingine unajisikia woga kwamba jamii sasa inategemea vitu vikubwa kutoka kwako, kwahiyo inazidi kukusukuma ufanye vitu vikubwa zaidi,” alisema
Tuzo kwa upande wa mitindo imechukuliwa na Jokate Mwegelo ambaye amesema amejisikia faraja kutambua kuwa kazi zake zinakubalika na ndio maana wamempigia kura.
Millard Ayo – Media
Richard Kazimoto – Uvumbuzi/Innovation
Ben Pol – Burudani
Ainaso Joakim – Arts and Designing
Michael Mbwambo – Ujasiriamali
Mgeni wa heshima kwenye tuzo hizo alikuwa ni Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia, Ndugu January Makamba. Makamba amewapongeza waandaaji wa tuzo hizo na kusema kuwa licha ya kwamba kuna changamoto za hapa na pale, wamefanya kazi nzuri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Youth For Africa (YOA), waandaaji wa tuzo hizo, Awadh Milasi amesema kutokana na kutoa tuzo hizo za kwanza, wamejifunza mengi na hivyo kuahidi kuzikuza zaidi tuzo hizo kwa kushirikisha mikoa mingine na nyanja nyingine ili kuzipa sura ya kitaifa.
Source:Jamii Forums