Like Us On Facebook

OFISA WA ZAMANI WA CCM ANAOMBA MSAADA....!!!

                                   Halfan Athuman

MKAZI wa Vingunguti Mtakuja mkoani Dar es Salaam, Halfani Athumani (65) anaomba msaada wa matibabu, kutokana na maradhi yanayomkabili.
Athumani ambaye kwa mujibu wake, aliwahi kuwa Katibu wa Wilaya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mikoa mbalimbali nchini, amesema ana maradhi ya maambukizi katika njia ya haja ndogo. Akizungumza katika ofisi za gazeti hili, alisema analazimika kutembea na mpira maalumu wa kupitishia haja ndogo.



Alisema kwamba ameugua kwa miaka miwili sasa na anahitaji Sh 700,000 za kutibu tatizo hilo. Kwa mujibu wa Athumani, aliwahi kufanya kazi katika mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Arusha, Tabora, Mbeya, Iringa, Morogoro na Dodoma kama Katibu wa Wilaya wa CCM.
“Mimi nimefanya kazi ya uongozi enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika wilaya nyingi, na baadaye nilipelekwa serikalini, nikafanya kazi Ofisi ya Waziri Mkuu kati ya mwaka 1988 hadi 1996 kama mhasibu, naomba viongozi waliopo madarakani sasa wanisaidie nitibiwe nateseka,” alisema. Alitaja baadhi ya viongozi aliowahi kufanya kazi nao ni Pius Msekwa.
Wengine aliowataja ambao wote ni marehemu ni Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Nje wa Tanganyika, Oscar Kambona, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa CCM, Rashidi Kawawa, Waziri Mkuu Edward Sokoine, Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba.
Athumani aliwaomba viongozi walioko madarakani wamsaidie kuokoa maisha yake. Ameomba wasamaria kuwasiliana naye kwa namba 0655331853 au kwa akaunti ya Benki NMB 2038300006.

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari