Like Us On Facebook

"ZIWA NYASA LOTE NI MALAWI, TANZANIA HAINA HATA PUNJE YA ENEO".... MGOMBE URAIS NCHINI MALAWI AFUNGUKA



Mgombea Urais wa Democratic Progressive Party (DPP) nchini Malawi, Peter Mutharika, amesema hakuna sababu za kufanya majadiliano kuhusu Ziwa Malawi ambalo Tanzania wanaliita Ziwa Nyasa.

 
Mutharika, ambaye ni mwanasheria, aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi  Mkoa wa Kati.
 Akikaririwa na gazeti la  Nyasa Times, Mutharika  alisema Tanzania haina cha kuambulia kwa Ziwa Malawi.



Kiongozi huyo ambaye hakuwapo katika mkutano wa Rais Joyce Banda na wapinzani kuzungumzia mustakabali wa ziwa, aliwahakikishia Wamalawi kuwa wasiwe na wasiwasi wa mvutano huo.
 

Mutharika ziwa lote ni mali ya Malawi na  akisisitiza kuwa, Tanzania haina hata punje ya eneo.
 

 “Hakuhitajiki majadiliano, Ziwa Malawi ni mali ya Malawi, litakuwa laMalawi,” alisema Mutharika ambaye alichukua masomo ya Sheria Tanzania.



 “
"Nitaleta meli Tanzania inatumia nafasi ya udhaifu wa uongozi wetu, lakini ukweli, hawana hata tone la eneo... Tutakapoitwa kwenye uchaguzi ujao mwakani, tutamaliza haya yote. 

nyingi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi, kutengeneza ajira za kutosha kwa vijana,” alisema Mutharika huku akishangiliwa na wafuasi wake.
 

Tanzania inataka kugawana ziwa, lakini Malawi imegomea mpango huo na suala hilo liko katika majadiliano ambayo Banda alisema kama mwafaka haukupatikana ifikapo Septemba 30, Malawi itapeleka suala hilo Mahakama ya Kimataifa (ICJ).

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari