Like Us On Facebook

NILIMPENDA SANA ELIKEM LAKINI MAMBO YAKABADILIKA!

MWAKILISHI pekee katika mashindano ya Big Brother The Chase kutoka Afrika Mashariki, Feza Kessy, amesema aliingiwa na fikra kwamba Elikem angekuwa mtu wa karibu yake, kwani waliingia ndani ya nyumba pamoja lakini mambo yalibadilika ndani ya siku 77 alizoishi humo.
Akizungumza na IK baada ya kutolewa ndani ya jumba hilo usiku wa juzi Jumapili, Feza alisema haikuwa rahisi kwake kutambua tabia halisi za Elikem mpaka alipokaa naye kwa muda mrefu ndani ya jumba hilo.

 
“Siku naingia ndani ya jumba niliongozana naye, nilimpenda kwa kumwona tu, lakini yeye bado sana kimapenzi,” alisema kabla ya IK kumrushia swali ‘Unampenda kweli Oneal?’, “ Ndio” alijibu Feza kwa sura ya aibu.
Feza alimweleza IK kuwa amekuwa akizozana mara kwa mara na Oneal kwa kuwa alihisi kwamba Feza alikuwa akimtumia jambo ambalo halikuwa sahihi.
Baada ya IK kumuuliza iwapo anadhani kuwa Oneal alikuwa na mwanamke mwingine akimsubiri nje ya jumba hilo, Feza alijibu; “Sina hakika na hilo.”
IK alipomuonyesha ni nani alimpendekeza kupigiwa kura za kutolewa, alishtuka baada ya kuona sura ya Dillish ikitokeza, hata hivyo Feza alisema ameshangazwa na kitendo cha Melvin kumpendekeza lakini alizungumza naye kabla kwamba alifanya hivyo.
Alipoulizwa anadhani nani atashinda, Feza alisema: “Siwezi kutabiri, lakini Angelo ni mtu ninayemhusudu zaidi.”
Wakati mpenzi wa Feza, Oneal, akitoka wiki iliyopita alisema: “Kazi niliyowahi kuipenda ndani ya BBA ni ndoa niliyofunga na Feza, niliifanya kama ndio kweli kwani nampenda sana yule binti” aliiambia Afrika.
Feza anaondoka ndani ya jumba hilo akiwa zikiwa zimebaki siku 14 tu mashindano hayo kumalizika, huku akiwa amewaacha washiriki saba wanaoendelea kuwania kitita cha Dola 300,000 (Sh 480 milioni)
Feza alipata kura nne kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Botswana. Cleo naye alipata kura nne kutoka Malawi, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe huku Dillish akiongoza kwa kupata kura saba kutoka Angola, Ghana, Ethiophia, Namibia, Nigeria, Sierra Leone na nchi nyingine za Afrika.
Cleo na Dillish wamefanikiwa kuendelea kubaki katika mashindano hayo baada ya kupata kura nyingi zaidi kuliko Feza. IK alifunga shoo kwa kuwataka washiriki waitumie siku ya Jumatatu (jana) kuwapendekeza wanaostahili kuondoka na wasiangalie urafiki wao.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari