Like Us On Facebook

MNUNUZI: REDIO YA SHARO IMENIFANYIA MAUZAUZA

Msanii  wa Kundi la Green Masage, linalorusha michezo yake kupitia Televisheni ya TBC, Daniel Mmasi ‘Face Brown’ amefunguka kuwa redio ya marehemu Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ aliyoinunua, imemletea mauzauza Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Daniel alisema alinunua redio hiyo ya ‘sabuufa’ kutoka kwa kijana aliyejulikana kwa jina la Suleiman (dalali wa mali za Sharo), lakini  anapoizima usiku, huwa inajiwasha yenyewe.
 “Niliichomoa kwenye umeme wakati wa kulala, ghafla usiku nikasikia inazungumza wakati sikuichomeka umeme, kuna siku nilikuwa narudi nyumbani kwa dirishani nikasikia inazungumza wakati asubuhi niliizima,” alisema Daniel ambaye ameamua kuirudisha redio hiyo kwa dalali bila kurejeshewa malipo yake.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari