Kwawadau wa vichekesho hapa nchini nadhani walio wengi wanamfahamu msanii huyu kutokana na umaahiri wake wa uchekeshaji kwa swaga za kimakonde, Wengi mnamtambua kwa jina ''Mapembe'' almaarufu ''Baba kundambanda'', Hususani wale mnaofatilia kipindi cha ''VITUKO SHOW'' kinachorushwa na runinga ya ''CHANNEL TEN'' Kila siku ya alhamisi saa mbili na nusu usiku au wale mnaofatilia filamu za vichekesho zinazoandaliwa na kampuni ya Al-Riyamy Production chini ya mkurugenzi wa kampuni hio ''Alphan ''Nassoro Abdala''. Baba kundambanda yuko hoi bin taaban kupitia ugonjwa ambao haujatambulika mpaka sasa! akiwa kambini Jijini Tanga huko wasanii wa kundi hilo walikoweka kambi ya takribani miaka miwili sasa,. Wasanii hao wa kundi la ''VITUKO SHOW'' wakiwa katika maandalizi ya kipindi na filamu za vichekesho, ndipo mwenzao alipoanza kuumwa gafla na kuzidiwa! mpaka sasa hali yake ni utata ila anaendelea kufatilia vipimo mwenyezi mungu atamjalia atapona na kuendelea na kazi kama kawaida hivyo wadau na wasomaji wa wetu muoombeeni Mungu amsaidie msanii wetu arudi katika hali yake ya kawaida ili azidi kuwavunja mbavu kama ilivyo ada.