Like Us On Facebook

MASTAA WALIODUMU ZAIDI KATIKA NDOA ZAO

IMEKUWA ni jambo la kawaida kabisa kuona ndoa za mastaa zikivunjika. Kashfa za ufuska pamoja na nyingine kadha wa kadha zimekuwa zikitajwa kama sababu za kusambaratika kwa ndoa hizo.
Pamoja na kuwako kwa idadi kubwa ya ndoa za mastaa zinazovunjika, wapo wengine ambao ndoa zao zimekuwa mfano mzuri, unapenda kuwafahamu?

Joke Silva
Ndoa ya mwigizaji Joke Silva ni miongoni mwa ndoa chache za Nollywood zilizoweza kukaa kwenye mstari bila ya mgogoro.
Tofauti na ndoa nyingine za Nollywood, ya kwake imeishi kwa kipindi kirefu bila kuwa na kashfa. Mume wa mwigizaji huyu, Olu Jacobs, ni nguli wa maigizo.
Ndoa yao inatajwa kuwa iliyojawa na furaha na baraka tele. Ndoa hiyo kwa sasa ina miongo mitatu na sasa Joke anaonekana kama kioo kwa wanawake wengi Nigeria hususan vijana.
Henrieta Kosoko
Ndoa ya Henrietta Kosoko nayo pia inatajwa kuwa ya mfano. Licha ya kuwa kwenye ukewenza lakini bado inaonekana kuwa ni ndoa imara kiasi cha kuhusudiwa na watu wengi. Siku zote amekuwa mwaminifu si tu kwa mumewe bali hata kwa jamii inayomzunguka jambo linalochangia kuiweka ndoa hiyo kwenye mstari ulio sawa.
Ngozie Orji
Ngozie Orji, mke wa mwigizaji, Zack Orji, naye anatazamwa kama kioo. Ndoa yao imedumu kwa muda wa miongo miwili sasa.
Katika kipindi hicho wamejaliwa kupata watoto watatu.  Kwa Nollywood ndoa yao inatajwa kuwa miongoni mwa ndoa zenye mafanikio makubwa sana.
Ireti Doyle
Akiwa ameolewa miaka kadhaa iliyopita sasa, penzi la Ireti kwa mumewe linaonekana bado lipo juu, kwani siku zote ndoa yao imekuwa ikionekana kama ndoa mpya.
Katika mahojiano yake aliyoyafanya hivi karibuni, Ireti hakusita kumwelezea mume wake kama ndio chanzo cha mafanikio ya ndoa yake.
“Kama mwanamke mfanyakazi, naondoka nyumbani kwangu kila siku saa kumi na moja asubuhi na kurudi usiku. Hiyo inaamanisha nyuma yangu kuna mtu anayekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha watoto wetu wamekwenda shule, huyo si mwingine ni mume wangu,” anasema. Kwa sasa ndoa ya Ireti Doyle inatazamwa kama kioo hususan kwa vijana.
Omotola Jalade-Ekeinde               
Omotola ni mwigizaji mwenye utofauti mkubwa na wenzake. Kwa kipindi kirefu sasa ameonekana kuwa mtaalamu zaidi katika masuala ya uhusiano wa ndoa.
Ndoa yake imekuwa ikitamaniwa na watu wengi. Hii ni kutokana na jinsi alivyokuwa na heshima, si tu kwa mume wake, bali hata familia yake kwa ujumla. Hii ni miongoni mwa ndoa iliyodumu bila kuwa na kashfa.
Omosexy kama mashabiki wake wanavyomwita, hivi karibuni katika moja ya mahojiano yake aliweka hadharani kuwa  penzi alilonalo kwa mume wake halikuja kwa bahati mbaya.
“Kila siku nimekuwa nikiwaambia watu kuwa wakati nakutana naye sikuwa nampenda, lakini kilichotokea lilikuwa ni penzi lililokuwa likichipukia, hivyo kadiri siku zilivyokuwa zikienda lilizidi kukua,” anasema.
“Nilivutiwa naye kutokana na ukomavu wake, nilikuwa na uwezo wa kujiona kwake, namaanisha ananijua kuliko ninavyojijua. Ukweli inatisha siwezi kuelezea. Huwezi kunielewa sawa. Lakini amekuwa akihisi maumivu yangu.”
Licha ya kukutana na mume wake huyo akiwa mdogo, amekuwa akithibitisha kuwa mume wake huyo ametoka kwa Mungu.
Ndoa yake hiyo sasa imetimiza miaka 16 huku wakijaaliwa kupata watoto wanne. Ni miongoni mwa ndoa zinazotazamwa na kila mtu nchini humo nayo inaitwa ndoa ya mfano.
Chioma Chukwuma
Ndoa ya Chioma pia ni miongoni mwa ndoa chache za mfano nchini humo. Ni ndoa iliyojawa furaha na amani siku zote. Licha ya uzuri na ustaa aliokuwa nao Chioma, amekuwa akiitanguliza ndoa yake kwanza halafu mambo mengine hufuata nyuma.
Hiyo ndio siri ya mafanikio yake kama anavyoeleza mara kwa mara staa huyo, yeye na mume wake wamejaaliwa kupata watoto wawili katika ndoa yao hiyo takatifu.
Oge Okoye
Licha ya umachachari aliokuwa nao Oge Okoye, amekuwa akiuthamini sana uhusiano wake wa ndoa. Kwa mara ya kwanza kabisa alikutana mume wake akiwa kwenye upigaji wa picha za filamu kwenye klabu moja nchini Nigeria.
Alisema mume wake huyo alipomwona alijua ni mmoja kati ya wasichana wa klabu kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa.
“Aliponiangalia kwa mara ya kwanza na mavazi niliyokuwa nayo siku ile, alivunjika moyo, lakini aliwaambia rafiki zake mmemwona yule msichana? Nitamtoa kwenye maisha yale na kumuoa. Hata hivyo rafiki zake hao walimwambia kuwa mimi ni mwigizaji na kwa wakati ule tulikuwa kwenye kuigiza. Tulibadilishana namba za simu na huo ukawa ndio mwanzo wa safari yetu,” anasema.
Watu wengi wamekuwa wakipenda jinsi Oge alivyokuwa na uhusiano mzuri kwenye ndoa na familia yake licha ya kuonekana kuwa hajatulia.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari