Like Us On Facebook

LUCY KOMBA, ROSE NDAUKA WAMNUNIA MONA, KISA..

                                                                  Lucy Komba.
MASTAA wa filamu Bongo, Lucy Komba na Rose Ndauka wanadaiwa kumchunia msanii mwenzao, Yvonne Cheryl ‘Monalisa’ kisa kikitajwa kuwa ni Prodyuza Mghana aitwaye Prince.
Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, awali Mona na Prince walikuwa washikaji na baadaye Mona akamtambulisha Lucy kwa jamaa huyo, hapo ndipo tatizo lilipoanzia.


“Lucy alipojuana na Prince, akamchukua Rose kisha wote watatu wakaenda Ghana eti kushuti filamu. Wakiwa huko sijui walimwaga sumu gani na hapo ndipo uhusiano wa Mona na Prince ulipoanza kufifia.
“Mona akashangaa ila akapotezea na hata Lucy na Rose waliporudi hawakuwa wakimchangamkia mwenzao, wakaanza kumchunia mpaka sasa,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzipata nyeti hizo, mwandishi wetu alimtafuta Mona ambaye alipopatikana alikiri kuwepo kwa ‘mnuno’ kutoka kwa wasanii wenzake hao, akasema chanzo ni Prince.  
“Niliamua kuachana na Prince kwa kuwa niliona ana tamaa na wasanii na nashangaa Rose na Lucy nao wanavyonichunia, ingawa kiukweli sikupenda kabisa kuongelea suala hili kwani sipendi shari,” alisema Mona.
Rose alipoulizwa alikuja juu na kudai hajawahi kuwa na ukaribu na Mona. Lucy hakuweza kupatikana kufungukia madai hayo.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari