Liyumba na mwanamke aliyedai ni mke wake, Aurelia Paulo Ngowi wamefikishana Mahakama ya Kinondoni, Dar kisa kikidaiwa ni mzee huyo kumtaka mwanamke huyo kuondoka haraka kwenye nyumba anayoishi na watoto wao wawili.Nyumba hiyo ipo Mbezi ya Afrikana, jijini Dar. Mbali na kuwa makazi, lakini sehemu ya mbele ya nyumba hiyo ni Hoteli Amjen yenye kupata wateja kila siku.Jina la Amjen linadaiwa ni muuganiko wa majina ya Amatus na Jennifer ambaye ni mtoto mmoja kati ya hao wawili wa mzee huyo. Aurelia ndiye aliyekimbilia mahakamani kuomba msaada ambapo shauri lake lilifunguliwa kwa namba 59, 2013 mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Rugemalira.Baada ya ombi hilo, mahakama ilimwamuru Liyumba kumwacha mkewe na watoto hao waendelee kuishi kwenye nyumba hiyo mpaka shauri hilo litakapotatuliwa kisheria.Haikujulikana mara moja kama Liyumba anataka mkewe na watoto waondoke kwenye nyumba hiyo na yeye kwa sasa anaishi wapi. Jitihada za kumtafuta zilifanyika, simu yake ya mkononi haikuwa hewani huku ikidaiwa kwamba namba husika haitumii tena.Baadhi ya watu wake wa karibu waliliambia Uwazi kwamba, kwa sasa Liyumba anaishi Kinondoni, Dar es Salaam lakini kupatikana kwenye simu ni ishu nyingine.