Like Us On Facebook

KICHWA CHA MTU ALIYEFARIKI DUNIA KIKIWA NA MIKONO MIWILI CHAKUTWA KATIKA OFISI YA MKUU WA POLISI NCHINI KENYA.

JESHI la Polisi Kenya lipo  katika uchunguzi baada ya kichwa cha mtu aliyeuawa kiliwa kimewekwa nje ya afisi ya mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya polisi Johnston Kavuludi jijini Nairobi.Kifurushi kimefungwa kwa karatasi ya plastiki, vilevile kilikuwa na mikono miwli ya binadamu iliyojaa damu. 


kando ya kifurishi hicho kulikuwa na ilaani iliyoandiskwa ''Kavuludi wewe ndiye utakayefuata''.Tangu uteuzi wake, kamishna huyo ameongoza harakati za kujaribu kuifanyia marekebisho idara ya polisi ambayo inadaiwa kuwa fisadi zaidi Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa idara ya polisi, hakuna mshukiwa aliyekamatwa kauhusiana na tukio hilo na kuwa bado wangali wanachunguza mwili huo ulikuwa wa nani.
Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na uhasama kati ya tume hiyo inayoongozwa na Kavuludi na ofisi ya mkuu wa polisi, huku zikilumbana kuhusu nani ana madaraka ya kuliendesha idara hiyo.
Source: Dj Sek Blog
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari