Like Us On Facebook

DR MWAKYEMBE AAGIZA WAFANYAKAZI WA UWANJA WA NDEGE WAKAMATWE KISA MADAWA YA KULEVYA

Dkt. Mwakyembe akionyesha picha ya Agness Gelard    "Masogange" kwa wanahabar
Ni Koplo Ernest, Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed ambao walihusika katika kuwasaidia Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa.Aidha, amesema wafukuzwe mara moja ni baada ya kupitia CCTV na kuona namna walivyohusika siku hiyo kwani walionekana wakipiga simu mara watoke nje kinyume na sheria za chumba cha ukaguzi (vifaa hivi ni kama vilivyotumika na CHADEMA kuwanasa polisi waliorusha bomu na baadae kuwashambulia kwa risasi).


Hao waliotajwa hapo juu ni waliofanikisha kupitisha kilo 180 zilizokuwa zimebebwa na wasichana wawili (Masogange na mwenzake) waliokamatwa huko Afrika kusini..
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe amewafukuza kazi na kuliagiza jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani ili kujibu mashitaka ya jinai, wale wote waliohusika katika kuuwasaidia Agnes Gerald na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Oliver Thambo nchini humo.

Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizaa yake kuhusu suala la dawa za kulevya
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari