Akizungumzia ishu iyo jana katika klabu ya Jacaranda iliyopo Kinondoni jijini Dar, Barnaba alisema hakwenda Kigoma ili amalizie arobabini ya mama yake.
“Siku ya Fiesta Kigoma ndiyo siku ya arobaini ya mama yangu na ndiyo maana unaniona niko hapa sijaenda Kigoma,” alisema Barnaba.
Uzinduzi wa tamasha hilo la Fiesta unatarajiwa kufanyika Jumamosi ya Agosti 17, mwaka huu mkoani Kigoma.