Like Us On Facebook

BOXER YAOKOA MAISHA YA MUME ALIYETAKA KUJIUA,MKE AMSHIKILIA KWA DAKIKA 20

 Alikuwa kwenye "apartment" yake ghorofa ya sita huko Changchun, China

                                Hapa akijitahidi na yeye kurudi ndani


Mke alimshikilia mume wake kwa dakika 20 kabla police na waokoaji hawajaja kumsaidia.


Majira ya saa moja na dakika arobaini asubuhi,jumatano mwanaume aliyetambulika kwa jina la Wang Li alitaka kujiua kwa kujirusha dirishani kutoka ghorofa ya sita anakoishi. Aliporuka tu mke wake alimuwahi kwa kushika boxer yake na baadae alimshika mguu akiacha upande mwingine unaoonekana ukining'inia dirishani.
Polisi waliitwa lakini polisi hao wanne wa kwanza walishindwa kufungua mlango. Baadae kwa msaada wa majirani waliweza kubomoa mlango na kumvuta baba huyo na kumrudisha katika hali ya usalama. Baadae walikuja kujua kuwa Wang Li mwenye miaka 45 alichoshwa na maisha ya kukosa kazi na ndio maana alitaka kujiua.

Mke wake alishikilia mguu wa mume wake kwa dakika 20 kabla msaada haujaja,sio mguu mdogo ukizingatia alikuwa na urefu wa sentimita 175 na uzito wa kilo 65.Majirani walikuwa wanachungulia madirishani ili waone tukio hilo.

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari