Like Us On Facebook

BAD NEWS : AJALI MBAYA YA BASI YAUA WATU 37 NCHINI MALAYSIA.....






Takribani watu 37 wameripotiwa kupoteza maisha nchini Malaysia katika mji mkuu wa nchi hiyo Kuala Lumpur(KL)  baada ya basi walilopanda kutumbukia katika korongo refu, maafisa wa usalama nchini humo wamesema ajali hii ni moja ya ajali kubwa ambazo zimewahi kutokea kutokana na kusababisha vifo vya watu wengi.

 
Baadhi ya abiria wameokolewa kutoka katika korongo hilo ambalo lina urefu wa futi 200 hali iliyosababisha waokoaji kutumia cranes pamoja na kamba kuweza kuokoa majeruhi wa ajali , ripoti kamili inaeleza kwamba basi hilo lilibeba abiria wapatao 49 na mpaka sasa ni abiria 16  waliokolewa wakiwa hai japokuwa hali zao bado no mbaya na huenda idadi ya vifo ikaongezeka, licha ya kutokea ajali iyo maafisa wa usalama wameshindwa kutambua uraia wa wahanga wa ajali iyo.


TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari