STAA wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amedhihirisha kuwa ni
sikio la kufa baada ya kusema yeye ni miongoni mwa wanawake wanaojua
kuchuna mabuzi.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Kauli hiyo imechochea vigezo vya kumfanya Shilole aonekane hasikii
kwani wiki kadhaa zilizopita mchungaji wa kanisa moja lililopo Ubungo,
jijini Dar ambaye hakujulikana jina lake, alimtaka kuishi katika sura ya
kumpendeza Mungu lakini inaonekana amempuuza.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi, jijini Dar es Salaam,
Shilole alisema alitunga wimbo wa Nachuna Buzi kwa sababu anajua kuwa
wanawake wengi ni mafundi wa tabia hiyo akiwemo yeye mwenyewe!
“Unajua
mwanamuziki unatakiwa kuchagua wimbo ambao unaigusa jamii nzima kwani
mambo ya kuchuna mabuzi kwa wanawake yapo sana, hata mimi mwenyewe ni
mtaalamu wa kuchuna mabuzi,” alisema Shilole.
Hata hivyo alisema japokuwa ana tabia hiyo lakini anatambua siyo
nzuri hivyo anawasihi wanawake wengine kuachana nayo kwani ipo siku
itawaingiza matatizoni.
Mbali na mchungaji huyo, juzi Jumapili, Mchungaji wa Kanisa la
Anglikana, Ukonga –Mazizini, Dar, Emmanuel Kapande alimtumia ujumbe wa
watoto wa Shule ya Jumapili (Sunday School) nyumbani kwake kwa lengo la
kuimba na kufanya maombi.
Watoto
hao walifika nyumbani kwa Shilole, Mwananyamala - Manjunju, wakiwa
wameongozana na walimu wao, Jonas Timotheo, Rehema Ezra na Catherine
Libogoma.
Ujumbe huo, ulimpelekea baraka ya maombi nyumbani kwake na kumshauri aishi katika mazingira yanayompendeza Mungu.
Katika
hafla hiyo, vinywaji baridi vilichukua nafasi yake huku Shilole akipata
nafasi ya kuzungumza na watoto hao kisha kupiga nao picha.
-GPL