MREMBO Asna Elias mkazi wa maeneo ya Manzese mkoani hapa, ameingia
matatani baada ya kutiwa mbaroni kwa wizi wa nguo za ndani za mgonjwa
aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Asna Elias akiwa mikononi mwa polisi baada ya kunaswa kwa wizi wa nguo za ndani.
Tukio hilo la aina yake, lilitokea Jumatatu iliyopita mchana wa jua
kali nyumbani kwa Kigogo wa UWT kupitia CCM, Bi. Mwajuma Malingo
anayeishi Mtaa wa Holowera Kata ya Mji Mpya.
Akizungumza na paparazi wetu kuhusu ishu hiyo, Malingo alisema kwamba
akiwa anaoga alisikia sauti ya vishindo vya mtu aliyekuwa akitembea.
Polisi akiangilia baadhi ya nguo za ndani alizokamatwa nazo Asna.
Kiongozi huyo wa UWT, alisema baada mtu huyo kusimama aliamua
kumchungulia kupitia tundu la funguo ndipo alimuona Asna akianua nguo za
ndani na nyingine ambazo zilikuwa mbichi na kuzisunda kwenye pochi na
mfuko wa rambo.
Asna akiwa chini ya ulinzi.
“Kama unavyoonaniko na khanga moja tu, nilikuwa bafuni naoga
nikasikia vishindo, nilipochungulia kwenye tundu la funguo nikamuona
huyu msichana anaanua nguo za mgonjwa aliyelazwa Hospitali ya Mkoa
ambazo nimetoka kuzifua sasa hivi, nikajifunga khanga na kutoka nje na
kuanza kumfukuza huku nikimwitia mwizi, cha ajabu na yeye alipaza sauti
kwamba hakuwa mwizi bali alinifumania na mume wake,” alisema Malingo.
Asna akiwa na aibu baada ya tukio hilo.
Malingo aliongeza kuwa, kufuatia mayowe ya mwizi aliyotoa, watu
walijitokeza na kuanza kumpa kichapo msichana huyo huku wengine wakitaka
kumchoma moto.
Wakati dada huyo akiendelea kula kichapo alitokea paparazi wetu
aliyewapigia simu askari wa kike waliokuwa doria ambao walifika na
kumtia mbaroni msichana huyo.
Asna akipewa vidonge vyao.
Askari hao walimpeleka Kituo Kidogo cha Polisi Kata ya Mji Mpya
akafunguliwa jalada la kesi namba MJ MPY/RB/18/2014 WIZI kisha kupelekwa
mahabusu ya kituo kikuu.
Asna akishushwa kituo cha polisi.
Aidha, Bi. Malingo alisema kwamba hivi karibuni amekuwa akiandamwa na
vibaka nyumbani kwake kwani wiki kadhaa zilizopita wezi walivunja
dirisha la chumba cha kijana wake Ally na kuiba redio ya ya shilingi
800,000, deki ya 200,000 na simu ya shilingi 100,000.