
VIDEO Queen mwenye figa matata Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’ 
amesema anaogopa kama ukoma kutembea na mume wa mtu kama wafanyavyo 
baadhi ya watu. 
 Agnes Jerald ‘Masogange’.
             Agnes Jerald ‘Masogange’.
 Akizungumza na paparazi wetu, Agnes ambaye hivi sasa amejiingiza 
kwenye soko la filamu, alisema anaogopa sana kuingia kwenye uhusiano na 
mume wa mtu ndiyo maana anaona bora aendelee na mpenzi wake wa siku zote
 kuepuka uhasama.
 
 
 “Sina
 tabia ya kushobokea kabisa waume za watu,  bora niendelee na mtu wangu 
wa siku zote na kama tukishindwana basi bora nitafute mwingine lakini 
awe wangu peke yangu,” alisema Masogange.


 
 
 
 
 
 
